Sisi asasi za kiraia na wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tumesikitishwa sana na mauaji ya kikatili ya watoto kumi (10) yaliyotokea huko Mkoani Njombe Januari, 2019. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi chanzo kikuu cha mauaji hayo inasemekana kuwa ni imani za kishirikina kwani miili ya watoto hao ilikutwa ikiwa imekatwa makoromeo na sehemu za siri.
Kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambavyo vinatweza utu wa mtoto kama binadamu, vinamkosesha mtoto ustawi na ukuaji bora na pia matukio haya yanapelekea kupoteza maisha kwa watoto wengi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa nusu mwaka 2018 kumekuwa na ongezeko la ukatili dhidi ya watoto ambapo jumla ya matukio 6376 ya ukatili dhidi ya watoto yaliripotiwa. Ripoti hiyo pia inatanabaisha kwamba katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018 watu 17 wanauawa kwa sababu ya imani za kishirikina ambapo hadi kufikia Juni 2018 jumla ya watu 106 waliuawa.
Watekelezaji wa matukio ovu dhidi ya watoto huwa wanawateka kisha kuwafanyia unyama na hatimaye kuwaua huku wakichukua baadhi ya sehemu za miili yao na kisha kuwatelekeza. Na ni dhahiri kwamba matukio ya utekaji hapa nchini yamezidi kushamiri licha ya jitihada mbali mbali zinazofanywa na jeshi la polisi pamoja na wananchi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola, kwa kipindi cha miaka mitatu watu wapatao 75 walitekwa. Waziri Lugola alikaririwa akisema licha ya juhudi za polisi nchini, mwaka 2016 kulikuwa na matukio ya watu 9 kutekwa lakini watano walipatikana wakiwa hai kwa ushirikiano na wananchi. "Watu wanne hawakupatikana, katika kipindi hicho na ambapo watuhumiwa sita walikamatwa; watano walifikishwa mahakamani na mmoja aliuawa na wananchi,"
Waziri Lugola alisema kwa mwaka 2017, watu 27 walitekwa na polisi walifanikiwa kuwapata 22 wakiwa hai na wawili wakiwa wamekufa, huku watatu wakiwa hawajulikani walipo hadi sasa. Katika kipindi cha "Januari hadi Oktoba 11, 2018, watu 21 walitekwa ambapo kati yao 17 walipatikana wakiwa hai na wanne hawakupatikana hadi sasa. Watuhumiwa 10 walikamatwa na kufikishwa mahakamani,"
Kuhusu utekaji wa watoto, Lugola amesema tangu mwaka 2016 ni watoto 18; (wakiume 6) na (wakike 12) waliokumbwa na adha hiyo. Aidha watoto 15 walipatikana wakiwa hai, wawili walipatikana wakiwa wamefariki huku mtoto mmoja akiwa bado hajulikani alipo hadi sasa.
Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuheshimu na kulinda haki za watoto, sambamba na kulinda haki ya kuishi kwa kuzingatia kwamba haki hiyo ni haki ya msingi kwa kila binadamu. Haki ya kuishi inalindwa na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kupitia Ibara ya 14. Hivyo basi kuvunja haki hii ni kukiuka Katiba pamoja na mikataba mbali mbali ya Kimataifa ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.
Pia, Tanzania imetia saini mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolinda haki ya kuishi na kutoteswa na pia Tamko la Haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo linalinda haki ya kuishi. Sheria ya Mtoto, 2009 kifungu cha 9 kinalinda haki ya kuishi na kifungu cha 13 kinalinda watoto dhidi ya matendo yanayotweza utu wao.
Pia ikumbukwe kuwa watoto ni kundi ambalo kwa namna moja au nyingine, hawawezi kupata baadhi ya haki zao bila kupata msaada wa wengine. Hivyo, jamii lazima iwe mstari wa mbele kulinda na kutetea haki za mtoto yeyote yule anayeonekana kuwa katika mazingira hatarishi na/ama ambaye haki zake zimevunjwa, zinavunjwa au inaelekea zitavunjwa. Tukumbuke kwamba; “mtoto wangu ni mtoto wako” na “mtoto wako ni mtoto wangu”
Mauaji yaliyotokea mkoani Njombe yanapaswa kukemewa vikali na kila mmoja wetu. Sisi asasi watetezi wa haki za binadamu tunawasihi Watanzania, wadau na Serikali kuheshimu haki za watoto na kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya kikatili kwa kufanya yafuatayo;
Wito wetu;
Mwisho tunatoa salamu za pole kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa haki ambao wameguswa na tukio hilo la kusikitisha na kuwaombea marehemu wote na Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amina.
Imetolewa Januari 31, 2019 na;
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

LEAVE A REPLY
Your email address will not be published.