Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesikitishwa na tukio la mauaji ya Bw. Peter Chambalo linalodhaniwa kufanywa na Mkurugenzi wa Wilaya ya ya Itigi Mkoani Singida Bw. Pius Luhende ndani ya Kanisa la Sabato siku ya Jumamosi Februari 2, 2019. Kitendo hicho ni uvunjifu wa haki ya kuishi kinyume na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inayoainisha haki ya kuishi kama haki ya msingi ya binadamu. Pia ni ukikwaji wa ibara ya 6 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, 1966 unaoainisha haki ya kuishi pamoja na kuweka jukumu la kulinda haki hiyo kisheria.
“kila mtu ana haki ya kuishi”
Kanuni ya utawala wa sheria inaweka sharti la kutumia utaratibu maalamu kwa mtu yoyote uliowekwa kisheria katika kutekeleza majukumu bila kujali cheo, hadhi au nasaba ya mtu. Kwa tukio hilo ni wazi kwamba, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi alijichukulia hatua mikononi bila kufuata misingi iliyowekwa kisheria katika kufanya jambo hilo. Pia, kitendo cha kuingia Kanisani kimeingilia uhuru wa kuabudu pamoja na faragha ya Kanisa hilo wakati wa kuabudu.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinalaani na kinakemea tukio hilo lililotweza utu pamoja na kuondoa haki ya kuishi ya mtu huyo. Kituo kinalaani tukio hilo kwani lilifanyika kikatili na kutia hofu na taharuki wakazi wa eneo hilo waliokuwa wamekusanyika kwa Amani wakifanya ibada siku ya Sabato. Kituo kinatoa rai kwa viongozi na watendaji wa Serikali kuzingatia misingi ya Katiba na sheria zilizopo katika kutekeleza majukumu yao.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinafuatilia kwa ukaribu tukio hili na kinatoa wito kwa vyombo vya dola kuendele kuchunguza na kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanatuhumiwa kwa mauaji haya.
Kituo pia kinatoa wito kwa uongozi wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Ikungi kuwahakikishia wananchi wa Itigi usalama wa maisha na mali zao na na kuhakikisha haki ya kuishi inalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Imetolewa Jumanne February 05 2019 na,
Paul Mikongoti
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

LEAVE A REPLY
Your email address will not be published.