Machi 8 kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kutambua nafasi na mchango wa wanawake katika kuchangia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani.
Umoja wa Mataifa (UN) uliridhia na kuanza kuadhimisha rasmi Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 1975 kwa lengo la kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia. Uamuzi huu ulifikiwa kupingana na mfumo dume ambao ulitamalaki katika jamii mbalimbali ulimwenguni na kuminya haki za wanawake.
Katika maadhimisho ya siku hii muhimu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaungana na jamii ya ulimwengu kutambua mchango wa wanawake katika kudumisha maendeleo endelevu. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinafanya juhudi kadha wa kadha kupambana na mitazamo hasi juu ya wanawake kwa kutoa elimu juu ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia kwa umma na kuwawezesha moja kwa moja wanawake kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya haki na usawa.
Kwa mwaka huu (2018) Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimejipanga kutoa msaada wa kisheria maeneo mbalimbali ya Tanzania ambapo tayari kuanzia Machi 1, 2018 tumeanza jijini Arusha katika kata za Kaloleni, Elerai, Themi, Sakina na Olemoti. Kwa jiji la Dar es Salaam tutakuwa Wilaya ya Kigamboni, kata ya Somangila na Kibada kuanzia Machi 7 hadi 9, 2018 na katika wilaya ya Ilala kata ya Mnyamani na Kitunda kuanzia Machi 14 hadi 16, 2018.
Sambamba na hilo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeandaa warsha itakayowakutanisha wanawake nchini kujadili na kufanya tathmini ya haki za wanawake, mchango na nafasi ya wanawake nchini.
Kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka 2018 ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”.
Your email address will not be published.
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

1 COMMENTS FOUND
zulfah msekayai Says:
March 3th ,2018 9:45 PMwanawake tunaweza