Kila mwaka, Februari 6 Tanzania huungana na jamii ya ulimwengu kuadhimisha Siku ya Kupinga Ukeketaji. Historia ya ukeketaji imeendelea kuwepo kwa takribani karne 21 sasa. Baada ya kutathmini kwa kina athari za ukeketaji kwa wasichana/wanawake na jamii kwa ujumla, mwaka 2003 Baraza la Umoja wa Mataifa lilidhinisha tarehe 6 Februari kuwa siku rasmi ya kupinga ukeketaji duniani.
Ukeketaji ni nini?
Ukeketaji ni kitendo kinachohusisha kukata au kuharibu sehemu ya uke wa mwanamke hasa kinembe kwa sababu zisizo za kisayansi. Kitendo hiki pia hujulikana zaidi kama tohara kwa mwanamke ambayo hutekelezwa kwa sababu za kiutamaduni.
Aina za Ukeketaji
Shirika la Afya Duniani limeelezea aina nne za Ukeketaji;
Aina hizi zote ni mbaya kwani zinamletea maumivu makali sana mwanamke anaekeketwa na kwa Tanzania aina ya kwanza na ya pili hutumika zaidi.
Sababu za ukeketaji
Jamii zinazoendeleza ukeketaji ni jamii ambazo zimetawaliwa na mfumo dume na mila kandamizi kwa wanawake. Sababu nyingi ambazo hupelekea utekelezaji wa kitendo hiki cha kikatili dhidi ya watoto wa kike na wanawake ni pamoja na:
Madhara ya Ukeketaji
Ukeketaji husababisha madhara makubwa kiafya kwa mtoto wa kike ikiwemo kupata athari za kisaikolojia kama msongo wa mawazo kwani watoto wengi hufanyiwa vitendo hivyo bila ridhaa yao. Madhara ya afya ya uzazi ambayo hupelekea kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua ni sehemu ya madhara yanayotokana na ukeketaji.
Madhara mengine ya ukeketaji ni pamoja na maumivu makali wakati wa ukeketaji, kumwaga damu nyingi na mara nyingine hata kupelekea kifo na maambukizi ya magonjwa hususani UKIMWI. Madhara ya muda mrefu ni kama; msongo wa mawazo, kovu la kudumu sehemu za siri, kutokufurahia tendo la ndoa, kupata shida wakati wa kujifungua na hata ugumba.
Hali ya Ukeketaji Tanzania
Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania inayotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu 2017, inaonesha kwamba pamoja na jitihada za wadau mbalimbali kutokomeza ukeketaji nchini bado mikoa kadhaa imebaki juu kwa takwimu za kitendo hicho cha kikatili kwa mtoto wa kike.
Kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey {TDHS} 2015-16 mikoa inayongoza kwa ukeketaji nchini Tanzania ni mkoa wa Manyara unaongoza kwa asilimia 58%, Dodoma 47%, Arusha 41%, Mara 32% na Singida 31%. Ripoti hiyo imefafanua pia kuwa vitendo vya ukeketaji hufanywa kwa asilimia 86% na mangariba au wakeketaji wa jadi na kuwa asilimia 25% ya wasichana hukeketwa kabla ya umri wa mwaka mmoja na asilimia 28% ya wasichana hukeketwa katika umri wa miaka 13 na zaidi. Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa hukeketwa pia na kuwa asilimia 95% ya asilimia 86% ya wanawake waliokeketwa hawakubaliani na kitendo hicho na wanatamani kisiwepo kabisa.
Ulinzi wa Kisheria dhidi ya Ukeketaji
Serikali kwa kushirikiana na wadau imendelea kuboresha sheria na sera kwa lengo la kukabiliana na ukeketaji na kuwajibisha wote wanaoendeleza mila hiyo kandamizi kwa watoto wa kike na wanawake.
Jitihada za Wadau
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kutokomeza ukeketaji hususani katika mikoa iliyotajwa kuongoza kwa ukeketaji na ukatili wa kijinsia. Kituo kimeendeleza kutoa elimu kwa jamii yote ili kukuza na kuimarisha uelewa wa kila mtu katika kupinga ukeketaji na vitendo vingine vya ukatili wa kijinsia. Ushirikiano baina ya Kituo na Serikali, taasisi za kidini, viongozi wa kimila, asasi za kiraia, vyombo vya habari na jamii kwa ujumla umepelekea kupungua kwa vitendo vya ukeketaji kwa mujibu wa tarifa ya TDHS.
Wadau kwa kiwango kikubwa wameendelea kupinga ukatili kwa watoto na wanawake ili kuendana na mikakati ya maendeleo endelevu ya kidunia na mikakati ya kitaifa ya kuondoa aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi watoto na wanawake. Juhudi za makusudi za Serikali bado zinahitajika ili kuhakikisha ukeketaji unatokomezwa kabisa na watekelezaji wa ukeketaji wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria husika.
Serikali inapaswa kuanzisha maeneo salama kwa ajili ya wasichana waliopo katika hatari, ya kukumbana na ukeketaji. Mipango ya sekta ya afya inapaswa kujumisha mikakati ya kuzuia na kutokomeza ukeketaji, kufanya marekebisho ya sheria ili kupiga marufuku ukeketaji wa wanawake walio zaidi ya miaka 18, kuimarisha Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji juu ya Utokomezaji wa Ukeketaji na serikali iendelea kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali na mashirika ya kimataifa kutokomeza ukeketaji.
Wito kwa Jamii Kutokomeza Ukeketaji
Kwa kuzingatia kauli mbiu ya maandimisho ya mwaka 2019 “Acha Mila zenye Madhara; Tokomeza Ukeketaji”. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinazisihi jamii hasa zile zinazoendeleza mila ya ukeketaji kuachana na mila hiyo isiyo na faida yoyote kwa wanawake na kwa jamii kwa ujumla.
Mwisho, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinavisihi vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali wanaoendelea kujihusisha na vitendo vya ukeketaji.
#TokomezaUkeketaji
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

LEAVE A REPLY
Your email address will not be published.