1) Mamlaka yaliyopitiliza anayopewa Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye masuala ya ndani ya chama
Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, 2018 unabadilisha jukumu la msingi la Msajili wa vyama vya siasa kutoka kuwa “msajili” mpaka kuwa “mdhibiti”. Mamlaka makubwa anayopewa Msajili katika Mswada huu yanafanya utekelezaji wa majukumu yake kwenda kinyume na misingi ya demokrasia na Katiba. Mswada unampatia Msajili mamlaka makubwa ya kudai taarifa – orodha ya wanachama, taarifa ya fedha ya chama, na “taarifa yoyote itakayohitajika.” Zaidi, ikiwemo mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya uongozi wa chama, kama orodha ya wanachama, kuweka vikwazo kwenye katiba za vyama, na masuala ya kinidhamu ya ndani ya chama.
Kwa kuzingatia kuwa msajili anateuliwa na (na anaweza kuondolewa na) Rais, ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala, hii inaleta mgongano wa kimaslahi. Msajili hapaswi kuwa na mamlaka kwenye masuala yanayohusiana na taarifa nyeti au mchakato wa kufanya maamuzi ndani ya chama, kazi yake ijikite katika kanuni za usajili wa chama.
Mapendekezo
2) Mabadiliko yazingatie kuwa sheria haijengi hofu au kupendekeza adhabu kali
Kwa kiasi kikubwa Mswada unafanya marejeo kwenye adhabu, hii inajitokeza karibu kwenye marekebisho yote. Suaal hili linajenga hali ya hofu wakati mtu anaposoma muswada, kwamba upo uwezekano wa kufanya kosa fulani.
Vilevile, adhabu zilizowekwa kwa makosa mengi hasa makosa ya kiutendaji hazilandani na makosa. Hazizingatii misingi ya kisheria, hususani misingi ya sheria za utawala na makosa ya kanuni za adhabu.
Ingawa vyama vya siasa vinapaswa kudhibitiwa, lakini vilevile, katika demokrasia changa, vinahitaji kulelewa. Kuanzisha mchakato wa kutoa maonyo, adhabu kali na kutokuoneshwa wazi utofauti uliopo kati ya makosa binafsi na makosa ya taasisi ni suala la kutazamwa kwa umakini.
Mapendekezo
- Kwa kiwango cha chini, majibu yanatakiwa kutolewa baada ya barua tatu za onyo kutumwa.
- Kama hakuna majibu yaliyopokelewa au hatua iliyochukuliwa kurekebisha kosa, chama ama taasisi inaweza kutozwa faini ambayo inayoendana na uhalisia.
- Kusimamishwa kwa muda, iwapo yafuatayo yamefikiwa: notisi ya maandishi ya
kutaka kukisimamisha chama ikiwemo maelezo ya kutosha kuhusu kosa lililofanyika, na nakala za barua zilizoandikwa na Msajili kukipa chama taarifa kuhusu makosa yake.
- Kufuta usajili iwapo makosa yameendelea kutendeka baada ya kipindi cha kusimamishwa kwisha, au pale inapotokea kutoridhishwa na majibu ya suala lililosababisha kusimamishwa.
- Uamuzi wa Msajili kufuta usajili wa chama uhusishe Baraza la Vyama vya Siasa na kuwepo na uwezo wa kukata rufaa mahakamani.
3) Kukandamizwa kwa haki ya uhuru wa kujieleza
Marekebisho yaliyoainishwa kwenye Mswada yamegusa maeneo matatu yanayoingilia haki ya msingi ya uhuru wa kujieleza .
Kwanza kuna katazo jipya kwa vyama vinavyofanya kazi kama vikundi vya uhamasishaji au vikundi vya harakati, vikundi hivyo vinaelezwa kuwa ni “vikundi vinavyoshawishi mitazamo ya wananchi au matendo ya serikali.” Kazi hizo ni msingi muhimu wa kazi za chama chochote cha siasa na hazipaswi kuzuiwa.
Pili, muswada umeainisha kuwa ni kosa kwa chama “kutoa kauli ambazo si za kweli” Kimsingi kifungu hiki kinatishia demokrasia na haki ya msingi ya uhuru wa kujieleza kwani ni ngumu kuainisha upi ni ukweli na upi ni uongo hasa katika masuala yenye utata hasa inapotokea mvutano wa kimtazamo au itikadi za kisiasa. Vifungu kama hivi pia vinaweza kusababisha kukosekana kwa usawa katika utekelezaji wa sheria.
Tatu, Mswada unampa malaka Msajili kuruhusu au kutokuruhusu elimu ya uraia na shughuli za kuvijengea vyama vya siasa uwezo.
Mapendekezo
4) Vikwazo pale vyama vinapotaka kuungana na kushirikiana
Marekebisho yamekuja na kanuni kwenye eneo ambalo hapo awali halikuwa limefafanuliwa kwa kina na sheria iliyoko ya Vyama Vya Siasa – suala la vyama kuungana na kushirikiana. Katazo hili jipya linasema kuwa vyama vitaruhusiwa kuungana “ndani ya siku 21 kabla ya kupendekezwa kwa wagombea wa uchaguzi mkuu” – kikwazo ambacho kinaweza kusababisha vyama vishindwe kuungana. Zaidi, na muhimu mno, Sheria inampa mamlaka waziri kutengeneza kanuni za kusimamia kuungana kwa vyama – huu ni mgongano wa wazi wa kimaslahi ukizingatia kazi ya waziri kwenye chama cha siasa.
Mapendekezo
5. Marekebisho ya sheria yametumia vifungu na maneno yasiyo na maana ya moja kwa moja ambayo kisheria yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja hivyo kuruhusu maamuzi yasiyo na usawa.
Baadhi ya vifungu katika sheria hii vinampa Msajili mamlaka ya kufanya maamuzi yenye madhara makubwa kwa vyama kwa kufuata kile “anachokiamini” au kwa “kutoridhishwa" na jambo fulani.
Mapendekezo
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

LEAVE A REPLY
Your email address will not be published.